CHURCH OF GOD
KUZALIWA MARA YA PILI
KIMETAFSIRIWA
NA
WAEMA J. MUTULU
Hiki kitabu sio cha kuuza!
Kimetolewa na church of God bila malipo kwa kuelimisha uma
© 1996 church of God
Uchapishaji wa hiki kitabu umewezeshwa na fungu la kumi la waumini, na michango ya
wale wasomi wa hivi vitabu vyetu ambao uchagua kushirikiana nasi katika hii kazi ya
kuieneza hii injili ya kweli kwa mataifa yote.
ambacho, mwanadamu wa kawaida hawezi kuamini, ndiyo, ni habari za urithi wa mwanadamu wa siku zijazo. Yesu hakuja akiongea mambo yaliyopita. Alionga juu ya mambo yajayo- yaani, ulimwengu ujao, ambao ni wa hakika. Hii pia ilikuwa ni habari kwamba, tunaweza kuzaliwa tena. Hata hivyo, karibu watu wote hawakuelewa maana yake. Ni wangapi leo wanajua ya kwamba, injili ya yesu haikuwa kwa njia yeyote dini mpya
au tofauti? Kwa nini haikutambulikana na walimwengu kama injili ya kutumainisha?
yamedanganyika kuhusu hii injili. Wakati ulikuwa umefika wa huu ujumbe kutangazwa. Sasa hivi ninapoandika wakati umefika wa ile maana yake kufafanuliwa kiasi ambacho watu
wataweza kuelewa Hii yote itaelezwa kwa hiki kitabu na ni kwako wewe unaokisoma.
Bwana, yule mnayemtazamia (masihi) atakuja kwa hekalu lake, Naam, mjumbe wa Agano – Mal 3:1”.
kidogo inataja malaki ambaye anaonyesha Yohana mbatizaji, akitayarisha njia mbele ya Bwana (mjumbe mwenyewe). Ukiendelea katika Marko 1:14-15; “Hata baada ya Yohana
kutiwa ngerezani, Yesu akaenda Galilayo akihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu, akisema, ” wakati umewadia na ufalme wa Mungu, umekaribia. Tubuni mkaiamini injil” – Yaani mkaiamini hii habari njema.
yenye watu, na 2) Serikali la hilo taifa. Mahali kwingine, utakuta kwamba watu wa taifa fulani ni uzao wa mtu mmoja. Jakubu aliitwa Israeli ambaye ndiye baba wa hilo taifa la Israel. Kabla
hawa mapacha hawajazaliwa, Mungu alimwambia mama yao Rebeka kuwa tumboni mwake kuna taifa mbili (Mwa.25:23). Yesu alikuja kama mjumbe wa agano. Agano la kale inaonyesha
wana wa Israeli kama taifa ama ufalme wa kibinadamu, ufalme wa Israeli. Yesu alikuja akitangaza ujumbe wa agano jipya ambayo inaonyesha ufalme wa Mungu wenye wana wa
Mungu wa kiroho. Kama vile ufalme wa Israeli ulikuwa jamii ya Yakubu, ndivyo ufalme wa Mungu utakuwa jamii ya Mungu, ambayo ni ya kiroho. Je, hii ina uhusiano gani na
“KUZALIWA MARA YA PILI”? Hiko uhusiano kubwa sana. Hebu tusikie.
wala watu wengine hawataachiwa enzi yake – nao utasimama milele na milele – Dan 2:44.”
milele ata milele.”
wetu, na wa Kristo wake; Naye atamiliki milele ata milele – Ufu 11:15.” Hata hivyo, baada ya maelezo kama haya, na katika vifungu vingine, wengi wa wahubiri waliodanganyika
wanahubiri kuwa kanisa ndiyo ufalme wa Mungu; Ama huu ufalme ni, siri isiyoweza kueleweka ndani ya moyo wako. Yesu alisema; wakati umewadia na ufalme wa Mungu ukaribu; Alimaanisha nini? Jibu lake inahitaji maelezo ya asili – ya kale.
na utukufu wa Mungu (Matendo 3:20-21). Swala ni hili, kulifanyika nini? Kwa nini ufalme huo hauko duniani sasa? Kwa nini hakuna amani duniani? Mwanzoni, wakati dunia iliumbwa, malaika walishangilia kwa furaha (soma – Ayubu 38:7).
ufalme wa Mungu. Kulikuweko na malaika mkuu – kerufi kwa jina la Lusiferi (maana yake, “aletaye nuru”). Alikuwa ni mmoja wa wale makerufi wawili ambao mabawa zao ufunika kiti
cha enzi cha Mungu. Lusiferi alikuwa amefundishwa vizuri sana juu ya utawala wa Mungu (soma ISA. 14:12-14; Ezek.28,12-17). Mungu utawala kwa njia ya amri zake ambazo ni za kiroho. Amri ambazo ni philosofia ya upendo – upendo kwa Mungu ambao ni kwa kujitolea na kutii hizo amri zake, pili upendo kwa viumbe wake-maisha ya kujali maslahi ya wengine na sio kujipenda tu. Kwa sababu ya ule urembo na hekima aliokuwa nao, moyo wa Lusiferi uliinuka, akashikwa na Kiburi. Kwa hivyo, alimkana Mungu, akawashawishi rnalaika waliokuwa naye na
kuwaongoza katika majaribio ya kipindua serikali ya Mungu, akiwa na kusudi la kutawala badala ya Mungu. Kwa sababu hii, Mungu aliuondoa utukufu wake, na tangu hapo ufalme wa
Mungu ukakoma hapa duniani. Lakini Lusiferi aliendelea kuitawala hii dunia kivyake, sio chini ya utawala wa Mungu. Lusiferi – aletaye nuru, aligeuka akawa shetani – mfalme wa giza, na malaika zake wakawa pepo wabaya. Kwa sababu ya dhambi ya malaika, dunia ilijaa giza na utupu (soma Mwa. 1:2). (Kwa maelezo zaidi, agiza kitabu chetu kiitwacho, “CHANZO CHA
KUASI). Kwa siku sita, Mungu aliiumba upya dunia (Mwa: 1:3-26), na akamuumba Mwanadamu.
Adamu, baba wa jamii ya binadamu, alichagua njia ya kuasi ambayo ni ya shetani; hivyo akashindwa kutawala mahali pa shetani. Yesu alipobatizwa na Yohana (Mark 1:9-11), Shetani
kwa ujasiri mwingi, alijaribu kumpotosha (Mark 1:12-13). Yesu alikuwa amekuja ili amshinde shetani na hivyo, arudishe ufalme wa Mungu hapa duniani ambao utaleta amani tena. Kama
vile Adamu alijaribiwa na akashindwa, na akafuata njia ya shetani, ilimbidi Yesu pia akutane na huyo shetani na kujaribiwa vivyo hivyo. Yesu alikuwa amekaa bila chakula kwa siku
arobaini wakati shetani alianza kumjaribu. Hata hivyo, katika huu udhaifu wa kimwili, alikuwa imara kiroho -Akamkana shetani kabisa.
kwa uaminifu. Mwishowe alithibitisha kuwa yeye ni mkuu kuliko shetani wakati alimuamrisha aende ambapo, shetani alitoweka (soma Mat.4:10). Alipomshinda shetani, alianza kutangaza
kuja kwa huo ufalme (soma Marko 1:14-15).
na tukapewa akili ambayo ni tofauti na ya Wanyama. Jamii ya mwandamu iliumbwa ili iweze kumpokea roho wa Mungu, na kuwa watoto wake. Katika mpango wa Mungu, alikuwa
amepanga iwe, kati ya kuja kwa Yesu mara ya kwanza, na hii mara ya pili, awachague wachache ambao watampokea roho mtakatifu, wapate kuelimishwa na kufunzwa kiroho kwa
njia ya neno lake ili watawale pamoja na Yesu akianzisha ufalme wake.
mbinguni ili aapishwe na hivyo kupokea mamlaka kutoka kwa Mungu. (7) Baada ya hayo yote, atarudi kwa hizo nguvu na mamlaka na, ataanza kutawala. Hizo ndizo, sababu, zilizofanya Yesu hasianze kutawala punde tu alipomshinda shetani.
wakuu alikuwa Nikodemu. Hawa wakuu walikuwa wanamchukia Yesu kwa sababu ya huo ujumbe. Nikodemu akiogopa kujulikana na wenzake, na hali akitaka kujua zaidi kuhusu huu
ujumbe, alimwendea Yesu usiku. Akamwambia; “Tunajua wewe ni mwalimu kutoka kwa Mungu.” Hii inamaanisha kuwa walimjua Yesu, na mahali alitoka. Lakini walikuwa watu ambao
nia yao ni kuhifadhi ukuu wao, na sio kupokea ufunuo wa Mungu.
Walifikiria wasipompinga, warumi wata-waondolea utawala wao na kuwaua kama waasi. Hii ni kwa sababu walifikiria Yesu ataanza kutawala mara moja (SomaYohana. 11:48).
kimwili, mbali wa watu waliovikwa kutokuharibika – jamii ya Mungu. Hivyo, alimwambia; “Mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa Mungu – Yohana 3:3.” Angalia kwa
makini tafadhali; kuzaliwa mara ya pili kuna uhusiano muhimu na ufalme wa Mungu, na vile huo ufalme sio wa wakati huu. Kumbuka, injili ya Yesu ni ya ufalme wa Mungu. Lakini, matamshi ya Yesu yalimshangaza Nikodemu. Wakuu wa dini, na mamia ya madhehebu na makundi wanaojiita wakristo leo wamedanganyika. Nikodemu alielewa maana ya kuzaliwa. Alijua ina maana ya kutoka tumboni mwa mama. Ina maana ya kuzaliwa katika ulimwengu huu kutoka tumboni. wakuu wa dini siku hizi wameigeuza na kuweka maana tofauti na hiyo. Kile
Nikodemu hakuelewa ni vile ingewezekana mtu mkubwa azaliwe tena, sio vile mtu uzaliwa. Kila mtu wa akili ya kimwili angeshangaa pia maana hufikiria kuzaliwa kimwili. Lakini
maana ya kuzaliwa inaeleweka kwa kila mtu.
inaonyesha kwamba, ufalme wa Mungu ni kitu mtu anaweza kungia, lakini mara tu akizaliwa tena. Sio wakati huu wa maisha ya kimwili Pia, Yohana 3:5 inaonyesha kwamba, ufalme wa
Mungu ni kitu mtu anaweza kuingia, lakini mara tu akizaliwa tena kuzaliwa kwingine lakini tofauti na kule kwa kwanza. Basi Yesu aliendelea kufafanua vile, ufalme wa Mungu sio wa wakati huu wa mwanadamu wa Kimwili. Alisema utakuja baada ya huu wa mwanadamu ni wa ulimwengu ujao.
damu. Wakati wa kuzaliwa, mtu utoka tumboni mwa mamake na kuingia katika ulimwengu. Wakati wa kuzaliwa mara ya pili, mtu atatoka tumboni mwa mamake wa kiroho (kanisa la Mungu) kwa njia ya kubadilishwa, na ataingia katika ufalme wa Mungu. Mtu sasa ni mwili na damu. Atakapozaliwa mara ya pili, atakuwa roho, sio mwili tena. Kuhusu huu wakati ujao, yesu alisema, “Hawaolewi wala kuowa, maana watakuwa kama malaika wa Mungu – Mat 7 22:30” Yesu alizidi kueleza akisema; “upepo uvuma vile upendavyo, na mtu usikia sauti yake, lakini huwezi sema utokako au uendako; ndivyo alivyo yeye aliyezaliwa kwa roho – Yohana. 3:8.” Uwezi kuona upepo. Hapa upepo ni mfano wa roho. Hii ndio sababu, mtu wa mwili, kama tulivyo sasa, hawezi kuona ufalme wa Mungu. Wale watakao urithi watakuwa
roho, watakuwa hawawezi kuonekana na macho ya kimwili.
mrithi na sio mwenye kumiliki. “Hii nasema wandugu, mwili na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu, wala kuharibika kurithi kutokuharibika -Wakor, 15:50” Ili afikie haya matamshi,
Paulo alikuwa ameeleza vizuri sana kuwa; “Mtu wa kwanza ni wa ardhi-mavumbi: mtu wa pili ni bwana kutoka mbinguni – roho -1 Wakor. 15:47” Na hii ndiyo Yesu alikuwa akimwambia
Nikodemu. Alikuwa mavumbi, wa dunia, alikuwa mwili na damu, sio roho. Alikuwa amezaliwa na mwili kwa hivyo, alikuwa mwili. Mtu akizaliwa na roho, anakuwa roho. Hii ndiyo Paulo
anafafanua hapa, Lakini sasa hatuwezi kuwa roho wakati huu. Kuzaliwa tena kuna wakati umewekwa. Endelea sasa na 1 Wakor. 15:” kama alivyo wa udongo, ndivyo walivyo walio wa
udongo – 48”. Hii ndiyo Yesu alikuwa akimwambia Nikodemu. Alikuwa amezaliwa na baba wa kimwili, alikuwa mwili na ndivyo tulivyo zote. Kifungu hicho kinaendelea: “na kama alivyo wa
mbinguni, ndivyo walivyo wa mbinguni.” Lakini kwetu wanadamu, itakuwa lini? Sio wakati huu. 1 Wakor. 15:49 – Na kama tulivyochukua sura yake yeye aliye wa udongo, kadhalika,
tutaichukua (wakati ujao) sura yake yeye aliye wa mbinguni.” Ndiyo; kama vile tulivyo mwili sasa, vivyo hivyo, tutakuwa roho – wakati wa ufufuo. Hapo ndipo tutazaliwa mara ya pili –
wakati tutauona, tuingie na kuurithi ufalme wa Mungu – (soma Mat. 25:34), wakati tutakuwa roho. “Sasa hii nasema wandugu, mwili na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu………..
Angalieni, nawaonyesha siri; sote hatutalala (kufa), lakini zote tutabadilishwa, ghafula, kufumba na kufumbua, wakati wa tarumbeta ya mwisho. Maana tarumbeta italia, na wafu watafufuka wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilishwa-1 Wakor 15:50 – 52”. Huu ndio ule wakati tulisema hapo hawali kuwa umewekwa. Wakati ambao tutaweza kuzaliwa tena – ambapo tutaweza kuona, kuingia na kurithi ufalme wa Mungu. Sio kabla ya hapo.
“Maana huku kuharibika (Mwili wa nyama) lazima kuvae kutoku- haribika (roho) na huku kufa sharti kuvae kutokufa.
Yaani, kubadilishwa kutoka mwili wa nyama na kuwa mwili wa kiroho. Kwa kifupi;
1. Mpaka tutakapozaliwa mara ya pili, hatuwezi kuuona ufalme wa Mungu.
2. Mpaka tutakapozaliwa mara ya pili hatuwezi kuuingia ufalme wa Mungu.
3. Mpaka tuwe roho, hatuwezi kuingia katika ufalme wa Mungu.
4. Wakati tuko mwili wa nyama, hatuwezi kuurithi ufalme.
5. Mpaka wakati wa ufufuo, wakati Yesu atarudi, hatutabadilishwa; hatuwezi kuwa roho.
6. Kwa hivyo, mpaka wakati wa ufufuo, hatuwezi kuuona, kuingia, ama kuurithi ufalme – hatuwezi kuzaliwa mara ya pili.
SASA TU WARITHI, SIO WAMILIKIO
Wakati huu tuko katika mwili wa nyama, hatuwezi kuuona, kuuingia, ama kuumiliki ufalme wa Mungu. Elewa vizuri sasa, hali ya wakristo leo katika haya maisha, katika ulimwengu huu.
“….. lakini mtu asipokuwa na roho wa Kristo, huyu sio wake – War, 8:9” Isipokuwa mtu ampokee roho mtatakatifu, na awe anakaa ndani yake, huyo sio mkristo. Kujiunga na dhehebu hakuwezi kufanya mtu mkristo. Kupokea na kufuata roho wa Mungu ndiko kunamfanya mmoja kuwa mkristo.
KUINGIA KWA ROHO MTAKATIFU KUNAFANANA NA KUINGIA KWA YAI LA MUME
NDANI YA LILE LA MKE
Sasa, ona vile kuingia kwa roho mtakatifu na kukaa ndani ya roho ya mtu kunaonyeshwa na vile yae la mume ya uzazi inapoingia ndani ya yai la mke na kuanza uhai mpya, ambao
unafanyika mtoto ambaye baadaye uzaliwa ulimwenguni. Yai la mume ikiunganika na la mke, mtoto hazaliwi mara hiyo – mbali huchukuliwa mimba. Uhai kutoka kwa yai la mume uingia
katika yai la muke lakini mtoto bado hajazaliwa. Katika hali hiyo hiyo, mtu akipokea roho mtakatifu (yai la uhai) kutoka kwa Mungu ambayo uingia katika akili yako (yai la muke), huyu
mtu hakui wa kiroho mara hiyo. Amechukuliwa mimba ya kiroho. Bado anangojea kukua katika neema na katika kumjua bwana ambapo akikomaa, hapo ndipo atazaliwa na atakuwa
roho. Tuendelee na warumi. “Lakini ikiwa roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yako, yeye — ataiuhisha miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa roho wake anayekaa ndani
yenu – War. 8.11.” Elewa hapa vizuri. Kuna uhusiano kati ya kuzaliwa kimwili na kuzaliwa kiroho. Uhai wa mtu wa kimwili uanza mara tu yai la mume ikishikana na yai la mke. Hapa
tunasema, mume amemtia mimba mke. Kufikia hapa kazi ya mume katika uzazi imekwisha.
Lakini, mpaka wakati mtoto huyo atazaliwa na mama, kuna kipindi cha miezi tisa. Ni muhimu kutoa huu mfano maana hapa ndipo uongo umejificha. Hapo ndipo wengi wanakosea wakifikiria kwamba; mtu akiisha mpokea Yesu, akiisha pata roho mtakatifu – tayari amezaliwa tena. Huu ni uongo. Elewa vizuri.
KIPINDI CHA MIMBA
Kutoka wakati ule yai la baba inaunganika na la mama mpaka wakati mtoto anazaliwa ni miezi tisa. Wakati huu, hutusemi mtoto amezaliwa. Yuko katika kipindi cha kuumbika ili
baadaye azaliwe. Wakati huu, huwa ni mtoto wa wazazi wake, lakini bado hajazaliwa. Katika kuzaliwa mara ya pili, hiki kipindi uanza mara tu mtu akimpokea roho mtakatifu. (Rudia War. 8:11 halafu fananisha na 1 Wakor. 15:50-53). Hii nataka ieleweke.
KANISA – MAMA YETU
Wakati mtu baada ya kutubu, kuamini na kubatizwa anampokea roho mtakatifu, roho wa Mungu umuingiza ndani ya kanisa lake. Hili kanisa linaitwa mwili wa Yesu. Kwa hivyo, tunasoma; “kwa maana katika roho mmoja, sisi sote tunabatizwa kuwa mwili mmoja – 1 wakor. 12:13.” Tena, hili kanisa linaitwa “Yerusalemu wa juu” (soma -waebr. 12:22-23).
Sasa ona Wagalatia 4:26 – Bali, Yerusalemu wa juu ni muugwana, naye ndiye mama yetu sisi sote.” Maana yake ndiyo hii: wakati roho wa Mungu anaingia ndani yetu, kwa kuingizwa ndani ya Kanisa lake, tunachukuliwa mimba ndani la hilo kanisa ambalo kwa sasa ndilo mama yetu. Mama anapomchukua mtoto katika tumbo, huwa anamlisha, anamlinda, ili akue kimwili – mpaka siku ya kuzaliwa. Huyu mama wetu wa kiroho kanisa “ulisha kondoo (1Petro 5:2) kwa njia ya utumishi wa wale Mungu ameteuwa,” kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu ………. hata mwili wa Knsto ujengwe………………. hata kufika cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo – Waefeso, 4:11-13”. Vile mtoto ukua kimwili wakati wa mirnba, ndivyo
tunakuwa kiroho ndani ya kanisa. Kanisa haiwalishi wakristo tu, mbali pia uwalinda kutokana na mbwa mwitu (wahubiri wa uongo) kwa kuwafundisha ile kweli, “ili tusiwe tena watoto
wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu – Waefeso 4:14. wakati wa ufufuo, sisi tulio katika kanisa, mama wetu wa kiroho, tutatoka tumboni mwake na kuzaliwa katika ufalme wa Mungu, jamii ya Mungu ambayo ni ya Kiroho.
SASA TU WANA WA MUNGU
Maelezo zaidi. “Kwa kuwa wote wanaongozwa na roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu – War. 8:14.”Mtoto ambaye bado yuko tumboni mwa mamake, ambaye bado hajazaliwa huwa ni mwana wa baba na mama yake. Ndivyo tulivyo sasa ikiwa roho wa Mungu anakaa ndani yetu; Ee, ikiwa ndiye anatuongoza. Lakini wakati huu, tumechukuliwa mimba, tu warithi lakini, bado hatujamiliki. Endelea: “Na kama tu watoto, basi, tu warithi, warithi wa Mungu warithio pamoja na Yesu, naam, tukitezwa pamoja naye ili tupate kutukuzwa pamoja naye War. 8:17.”
Sasa, ona vile hiki kifungu kinaonyesha mpango wa ufufuo kuingia katika utukufu – wakati tutakuwa roho na ni kwa njia ya kuzaliwa. “Kwa maana viumbe pia vinangojea kwa shauku
nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu;” Huu ni wakati Yesu atakuja kutawala, na wakati watu wa fufuliwa au kubadilishwa, (kuzaliwa) navyo vitawekwa huru, na kutolewa katika utumwa
wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa wana wa Mungu – War. 8:19-21”. Si hili jambo imekuwa wasi kabisa sasa?
Hapo kuna mfano mwingine. Tutawekwa huru kutokana na maisha haya, (kanisa sasa iko hapa ulimwenguni ijapokuwa sio la ulimwengu) na kuingia katika ulimwengu ujao wa utukufu. Viumbe wanangoja wakati huu ambao Yesu atakuja, watu
watafufuliwa, na ufalme wa Mungu utatawala. Kwa maana viumbe watawekwa huru kutokana na uharibifu. (Hawajawekwa huru sasa, lakini watawekwa wakati ujao), wakati wa ufufuo. Wakati wa ufufuo ambao tutabadilishwa tuwe roho na kuingia katika ufalme, na ni wakati pia wa kuwekwa huru kutokana na miili ya uharibifu na, kutoka kwa huu ulimwengu – (maisha) wa dhambi – yaani, kuzaliwa kwenyewe.
YESU AZALIWA MARA YA PILI KWA NJIA YA UFUFUO
Endelea na Warum. 8:29 – Maana wale aliowajua tangu mwanzo, aliwachagua wafananishwe na mwanawe, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.” Sasa, fananisha hicho kifungu na Warumi 1:3-4; “habari za mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili, na kudhihirishwa kwa uwezo kuwa mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho wa utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu.” Katika kuzaliwa mara ya kwanza, Yesu alikuwa na mwili wa kibinadamu, alikuwa mtoto wa ukoo wa Daudi, Lakirii
alizaliwa mara ya pili wakati alifufuka kutoka kwa wafu akawa mwana halisi wa Mungu, mwenye mwili wa roho. Basi, yeye alikuwa wa kwanza kuzaliwa kwa njia hii ya kufufuliwa,
miongoni mwa wandugu wengi ambao pia watafufuliwa kama yeye siku ya mwisho (soma Yohana 5:28-29) na kuwa viumbe wa kiroho……….ndiyo, na kuzaliwa mara ya pili. Eee, kwa
kuandika hayo, tumeelewa kuwa, wakati Yesu alikuwa katika mwili, alikuwa pia ni mwana wa Mungu maana uhai wa roho mtakatifu (yai la uhai la Mungu) ulikuwa ndani yake. Lakini hii
inaonyesha kuzaliwa kwa aina mbili. Moja ya kimwili kupitia kwa Maria mamake, wa ukoo wa
Daudi, na ya pili, kwa njia ya ufufuo katika utukufu, kuwa mwana wa Mungu, kwa kufufuliwa naye; na sisi sote tulio katika Kristo, ambao roho wa utukufu anakaa ndani yetu, twaweza
kuzaliwa vivyo hivyo, Hii haimaanishi kwamba Yesu alikuwa mwenye dhambi. Yeye kwa kuishi haya maisha ya kimwili hata kufa na kufufuliwa, alikuwa anatuwekea mfano, wa ule mpango tutapitia kabla hatujafikia ukamilifu.
TUKIZALIWA TENA, TUTAFANANAJI?
Jibu ni hili: WafilipI 3:20-21 – “kwa maana Wenjeji wetu uko mbinguni, na kutoka huko, tunamtazamia mwokozi bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate
kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uwezo ule ambao, aweza kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake”. Kama tutafanana naye; mwili wake wa utukufu unafananaji? “Macho yake ni
kama miali ya moto, uso wake ni kama jua ing’aavyo mchana (soma.Ufu. 1:14-16)”
WAKATI HUU TUMECHUKULIWA MIMBA LAKINI BADO KUZALIWA:
Kama vile kuzaliwa kimwili kunachukuwa muda, mifano na vifungu vimeshuhudiwa kiasi cha kuaminika kwamba kuzaliwa mara ya pili pia kunachukua muda. Wakati yai la baba
linaunganika na la mama, mama uchukua mimba. Huku kuunganika kwa haya mayai mawili kunaanza uhai wa mtoto tumboni mwa mama, lakini hazaliwi mara hiyo; na hazaliwi mpaka baada ya miezi tisa. Hata hivyo, wakati huu wa kukua kwa mtoto ndani ya tumbo ya mamake, yeye huwa ni mtoto wa wazazi wake ijapokuwa hajazaliwa bado. Kwa njia hiyo hiyo, wakati baba wa roho (Mungu) anaweka roho mtakatifu ndani ya akili ya mwanadamu, huyo mtu huwa ni mtoto wa Mungu aliye ndani ya tumbo. Yeye huwa bado ni mwili wa nyama. Lazima
aumbike kiroho, ki-tabia za Mungu (2 Petro 3:18). Yeye yuko katika ile hali ya kuumbika UMungu, ili akiimarika, aweze kuzaliwa, na ni kwa njia ya kufufuliwa na kubadilishwa. Kwa sasa, yeye yuko kwa mimba ya Kanisa la Mungu hapa duniani (soma. 1 Wakor 4:1). Kwa sasa, wale walio katika kanisa la Mungu ni wana wa Mungu wa mwili wa nyama. Vile tuliona, damu na mwili haviwezi kuuona, kuuingia au kurithi ufalme wa Mungu. Ufalme wa Mungu ni wa wana wake ambao wamekwisha kuwa roho. Wote katika kanisa ambao wana roho mtakatifu wako katika hali ya kutayarishwa ili wazaliwe kiroho. Hawajazaliwa bado wala hawajaingia katika ufalme.
UWEZO MKUU KULIKO NGUVU YA UPEPO
Kuna ukrasa mwingine ambao karibu watu wote hawauelewi, na ambao unaonyesha vile tutakuwa baada ya kuzaliwa tena, Unaanza katika Waebrania 2:6. Lakini kwanza, tuone kuhusu
Yesu katika Waebr, 1:1 -3”. Mungu ……….. mwisho wa siku hizi amesema nasi katika mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye, aliufanya ulimwengu. Yeye kwa kuwa ni
mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichua vyote kwa amri ya uwezo wake” Mamlaka yote (soma- Mat, 28 18) yamepewa Kristo Yesu.
Yeye ndiye afisa mkuu katika ufalme wa Mungu, Sasa tuendelee katika – Waebrania 2:6 “Mwanadamu ni nini hata umkumbuka?” Ndiyo, ya nini Mungu ashughulike, na mwanadamu? Kwa nini alituweka hapa duniani? Maisha yana kusudi gani? Sababu yake ni kuu kushinda vile umewahi kudhania wakati wowote ule. Uko tayari kuamini kile tutaeleza hapa? Basi sikiliza vizuri hili jibu la kusisimua. Fungu la 7. La Waebra.2. Umemfanya mdogo punde kuliko malaika, umemvika taji la utukufu na heshima. Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako” – yaani juu ya uumbaji wa Mungu wote.
HAYA MAMLAKA BADO KWA SASA
“Umeweka vitu vyote chini ya nyayo zake. Kwa maana kwa kuweka vitu vyote chini yake, hukubakisha kitu kisicho chini yake”. Unaweza kufikiria hiyo? Yaani, vitu vyote-jua, nyota,
bahari na anga, juu ya ulinzi wako! Lakini hii ni kwa wana wa Mungu ambao ni wa Kiroho.
Kwa sasa, mwanadamu hajazaliwa (hajakuwa) bado. Yesu peke yake ndiye amezaliwa na kufikia hayo mamlaka. Tuendelee fungu la 8………… “Lakini, bado vitu vyote kuwekwa chini ya
mwanadamu.” Tunaona nini sasa? fungu la 9.” Ila, twamwona…………Yesu amevikwa taji la utukufu na heshima.” Ndiyo, kama vile tuliona katika Waebr. 1: Yesu tayari amekwisha
fanywa mkuu wa ufalme wa Mungu. Lakini kwa sasa, amemwacha shetani aendelee kutawala mpaka wakati wetu wa kumiliki ufike, wakati Yesu atarudi. Tuendelee. “Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake, vitu vyote viliumbwa, akilete wana wengi, Waufikilia utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya matezo. Maana yeye atakazaye na hao wanaotakazwa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake – Waebr. 2.10-11”
YESU MZALIWA WA KWANZA, MIONGONI MWA WENGI
Kama tulivyoona awali, sisi tu warithi wa Mungu, warithio pamoja na Yesu kama nduguze. Alitangulia kuishi haya maisha tunayoyaishi, na yale tunayongojea, kama mwanzilishi. Yeye
peke yake amezaliwa mara ya pili, na sisi pia tulio ndugu zake tunangojea kuwa kama yeye (1Yohan 3:2). Yeye amekwisha miliki vitu vyote, lakini sisi bado tuwarithi, tunaendelea kuumbika
ndani ya turnbo hata tuwe tayari kuzaliwa kama yeye. tupate kumiliki kama yeye pia. Kwa sasa, yeye aliyekamilika (Yesu) ni kuhani wetu mkuu, anayeshungulikia vile tunakuwa Kiroho, huku
akitutayarisha kuwa makuhani na wafalme, ili tutawale pamoja naye. Kwa miaka elfu moja ya kwanza Yesu akija, tutatawala dunia. Maana atakuwa, “amewafanya wafalme na makuhani
………… nao wataimiliki dunia – ufunuo 5:10”.
MIAKA ELFU MOJA YA KWANZA
Kwa miaka ya kwanza elfu moja, Yesu atatawala juu ya kiti cha enzi cha baba yake wa kidunia – Daudi hapa Yerusalemu (soma Isa.9:6-7), “Na yeye ashindaye na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma -Ufunuo 2:26-21′.” Lakini, tutatawala kivipi, na kutoka wapi? Yesu anajibu. “Yeye
ashindaye nitampa kuketi nami katika kiti changu cha enzi (Yerusalemu) kama vile nilivyoshinda nikaketi pamoja na baba katika kiti chake cha enzi – ufu 3:21.”
Tukiisha zaliwa na Mungu, tutakuwa roho, sio mwili na damu tena. Tutapewa uwezo, kama vile Danieli anaonyesha kuwa; “watakatifu watazichukua, falme za mataifa ya dunia hii na
kuzitawala.” Baada ya hapa, Waebrania 2:8 inaonyesha kuwa utawala wetu utapanuka hata uifikie mbingu ………….. vitu vyote. Maana haya ndio mamlaka na uwezo aliyepewa yeye
aliyeitimu, yaani Yesu Kristo ambaye tutafanana naye.
LAZIMA TUKUE WAKATI HUU WA MIMBA
Uhai wa mwanadamu uanza na kile Biblia huita, “mbegu iharibikayo” yae la mume ya kimwili. Uhai wa utukufu uanza na kile kisichoharibika – roho ya Mungu kuingia ndani ya roho ya mwanadamu. Vile mimba ukua mpaka iumbike iwe mwanadamu ndio izaliwe katika jamii hiyo ya mwanadamu, ndivyo mkristo ambaye ndani yake roho wa Mungu (yai la uzazi) anakua. Imempasa kukua hata aumbike viungo vya Mungu, ili akikomaa (soma Waefeso 3:19), aweze kuzaliwa katika jamii la Mungu. Atakuwa mkamilifu ambaye hawezi kutenda dhambi. Petro anaonyesha vile huu mpango unaendelea akisema, “kwa kuwa mnazaliwa mara ya pili (mnaendelea kuumbika ili baadaye mzaliwe), si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa isiyoharibika, kwa neno la Mungu lenye uzima lidumulo hata milele – Petro 1:23.”
ukiendelea 1 Petro 2:2 – kama watoto wachanga waliozaliwa sasa ………..” Hapa, Petro hasemi tumezaliwa tayari. Anafananisha kukua kiroho na vile mtoto aliyezaliwa ukua. Hasemi eti, tayari tuwazaliwa wadogo katika ufalme wa Mungu. Lakini anasema “kama vile mtoto mdogo ukuwa” nasi takue vivyo hivyo kiroho. Hii ni njia ya kueleza vitu vina -vyofanana, sio eti, viko sawa. Kwa hivyo anaonyesha vile tunahitaji kula katika neno ikiwa tutakua.
KIFANANISHO
Tunapoongoka (yaani kumgeukia Mungu na kumpokea roho mtakatifu) na kuanza maisha ya Kristo (soma, Warumi.8:9), huwa tayari tumekuwa wana wa Mungu (soma Waru. 8:14),
lakini wana ambao hawajazaliwa, ambao bado wako tumboni, huwa, Mungu amepanda ndani yetu mbegu ya uzima wa milele, hii ikiwa ni thibitisho kuwa atatupa huo uzima tukiisha komaa
(soma Waef. 1:13-14). Bila Mungu, sasa hivi (ijapokuwa tumeongoka, tuna roho mtakatifu) hatuna uzima wa milele. Tunategemea Mungu kwa njia ya Kristo kwa uwezo wa huyu roho mtakatifu. Mungu aliahidi kwamba, atatupa huo uzima wa milele. Lakini huu uzima ni kitu mtu anaweza kupoteza. Kama vile mimba wakati mwingine utoka mtoto akakosa kuzaliwa, ndivyo ilivyo kwa wakristo, Kama vile uhai wa mtoto ndani ya tumbo utegemea mama yake, na kuingia kupitia kwa kitovu, ndivyo mkristo wa kimwili upata uhai wa roho mtakatifu kupitia kwa Yesu Kristo aliye Kanisa, ambayo ndio mama yetu.
Maandiko matakatifu yanaeleza vizuri sana, yanaposema; “ Na huu ndio ushuhuda kwamba Mungu alitupa uzima wa milele, na uzima huu umo katika mwanawe. Yeye aliye na mwana, anao huo uzima, asiye na mwana, hana huo uzima – 1 Yohana 5:11-12 ”. Unaona! Sasa hatuna huu uzima ndani yetu pasipo kutegernea
mama yetu …………….. yaani kanisa ambayo ni Yesu. Uhusiano wetu na Yesu kupitia kwa roho mtakatifu ndio mfano wa vile mtoto aliye ndani ya tumbo uhusiana na mama kupitia kwa
kitovu cha huyo mtoto. Mtu akitengwa na Kristo, hawezi kuendelea kuwa na huyo roho mtakatifu (uzima wa milele). Mtoto akiisha zaliwa huwa ana uhai ndani yake. Hategemei uhai
wa mama tena. Anakuwa kivyake sasa. Hii inaeleza vizuri tofauti iliopo kati ya kuchukuliwa na kuzaliwa. Wakati tutazaliwa mara ya pili, tutapewa uzima wa milele.
Hatutategemea tena kwa Yesu, maana tutakuwa kama yeye; “Maana kama vile baba alivyo na uzima nafsini mwake – Yohana 5:26”. Kwa sasa, bado hatujakuwa katika hali hii.
VILE YESU NDIYE MZALIWA WA PEKEE
Mfalme Daudi alikuwa na roho mtakatifu. Alipokuwa akitubu mbele za Mungu baada ya kuzini na Bathsheba na kumua, Uria, aliomba; “Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu. Usinitenge na uso wako, wala roho wako mtakatifu, usiniondolee – Zaburi 51:10 – 11″ Manabii walimpokea roho mtakatifu, maana juu yao, Petro anaandika; “………. watakatifu wa Mungu waliongea wakiongozwa na roho mtakatifu –2 Petro 1:21.” Hawangeitwa watakatifu kama roho ya Mungu haikuwa ndani yao. Ibrahimu, Isaka na Yakubu wataonekana katika ufalme wa Mungu. Kwa hivyo, roho ya Mungu ilikuwa ndani yao.
Walichukuliwa mimba na Mungu lakini hawakuzaliwa, maana Yesu ndiye mzaliwa wa kwanza miongoni mwa wandugu wengi. Manabii na waandishi wote wa Biblia walichukuliwa mimba kwa kumpokea roho mtakatifu, vile kila mkristo katika kanisa la Mungu alivyo leo. Lakini hata wa leo, bado hawajamiliki, ama kuingia katika ufalme wa Mungu, maana bado hawajazaliwa mara ya pili. Yesu alikuwa wa kwanza kuzaliwa na Mungu Miongoni mwa wandugu wengi ambao, watazaliwa wakati wa ufufuo; maana imeandikwa, “Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi (hawakuzaliwa tena, bado-kumiliki ufalme): Kwa kuwa, Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi – Waebr. 11:39-40”. Hii bado inaendelea kuthibitisha kwamba, kuongoka, kupokea roho mtakatifu katika maisha haya ya mwili wa nyama, sio
kuzaliwa tena mbali ni kuchukuliwa mimba. Maana, ijapokuwa manabii walikuwa mbele ya Yesu, na walikuwa na roho mtakatifu, hawa-kusemekana kuwa wamezaliwa tena. Yesu peke
yake ndiye amezaliwa hii mara ya pili kwa njia ya kufufuliwa kutoka kwa wafu. Hatua za kuzaliwa mara ya pili zinaendaji?
NJIA NI GANI?
Petro alieleza hiyo njia na masharti yake alipowaambia wayahudi; “Tubuni, mkabatizwe”, kama onyesho la kumwamini Yesu, na damu yake iliyo mwagika kulipia dhambi zetu, na kuamini ufufuo wake ambao unawezesha mtu kuzaliwa tena na kupokea uzima wa milele.
Basi mmoja akiisha kufanya hayo, Petro alisema, “nanyi mtampokea roho mtakatifu.” Wale ambao roho mtakatifu anakaa ndani yao ni wa Kristo. Wale wengine sio wake. Ikiwa roho ya
Mungu inakaa ndani yao, Mungu (kama vile alimfufua Yesu kutoka kwa wafu), atawafufua na kuwapa kutokuharibika – uzima wa milele, kama vile alimpa Yesu. Haya maandiko yote
yanaonyesha wasi kuwa tutazaliwa mara ya pili, kwa njia ya kufufuliwa peke yake, ambapo, tutabadilishwa na kuvishwa miili ya roho isioweza kufa. Sasa tuwarithi, warithio pamoja na
Kristo, bado hatujamiliki huo ufalme.
KUZALIWA KIMWILI
Kuzaa ni nini? Kuzaliwa kuna maana gani? Huku sio kwingine ila mtoto kutoka tumboni mwa mama na kuja ulimwenguni. Lakini huku kuzaa kunahitaji baba na mama. Kama sio yai la baba kuunganika na la mama, hakungekuwa na mtoto. Wakati huo Muungano unafanyika, hatusemi mtoto amezaliwa mbali tunasema, mama amechukua mimba. Kuanzia wakati
mimba imechukuliwa, kwa muda wa miezi tisa, huyu mtoto uumbika viungo vya mwili na baada ya hapo, huwa yuko tayari kuzaliwa.
Hivyo ndivyo inafanyika katika kuzaliwa kiroho. Mtu anapobatizwa, upokea roho mtakatifu. Huyu roho ni nguvu za uhai (yai) za Mungu. Kusema umezaliwa mara ya pili baada ya
kumpokea roho mtakatifu ni sawa na vile, mama akipata mimba anaweza kusema amezaa; na ni wasi atakuwa anadanganya. Hivyo, elewa kuwa, ukipokea roho wa Mungu, kwa muda wote huu wa maisha haya tunayoishi katika mwili huu, uko tumboni ukiendelea kuumbika kiroho (soma 2 Petro. 3:18) ili Yesu akija, Eitha, kwa njia ya kufufuliwa au kubadilishwa, uzaliwe kutoka kwa kanisa na kuingia katika ufalme wa Mungu, ukiwa roho kama vile baba yako alivyo roho. Kuzaliwa kimwili huwa tuko mwili. Tukizaliwa Kiroho tutakuwa roho.
HALI YA WAKRISTO SASA
Yesu alipokuwa akizungumza na Nikodemu, alikuwa akiongea juu ya wakati ambao Wakristo wataweza kuzaliwa tena na hivyo kuona na kuingia katika ufalme wa Mungu. Kwa vile ufalme
wa Mungu ni jamii ya Mungu. Wakati huo tutazaliwa kuwa wa jamii hiyo na kufanana na baba yetu. Sasa tukiunganisha haya maelezo na 1 Wakori. 15:45-53, imekuwa dhairi kuwa
hatuwezi miliki ufalme wa Mungu tukiwa katika mwili huu, mbali baada ya kufufuliwa na kuwa viumbe wa roho. Kuzaliwa mara ya pili ni wakati huo wa ufufuo. Kwa sasa, wakristo wako katika kipindi cha kuchukuliwa mimba. Hata hivyo ni wana wa Mungu, maana hiyo mimba ni kwa uwezo wa roho wa Mungu.
JAMBO MUHIMU
Ni mafundisho ya wakatoliki kwamba kanisa ndiyo ufalme wa Mungu. Mtu akifuatia hii imani ya wakatoliki, inamaanisha yeye akiisha kuwa muumini wa hilo kanisa, tayari ameingia katika ufalme wa Mungu. Na kwa vile hawezi kuingia katika huo ufalme akiwa mtu wa kawaida, wanaamini kuwa, mtu akiisha pata roho mtakatifu, amezaliwa mara ya pili. Wa protestanti wamefuatia hii imani ya katoliki, ijapokuwa wengine ufikiria kuwa ufalme wa Mungu ni kitu kilicho moyoni mwa mtu, Watafsiri wengi wa Biblia walikuwa watu wa imani hii, Kwa hivyo, walitafsiri vibaya hili neno la kigiriki “Gennao” kuchukuliwa mimba, na kuipatia maana ya kuzalrwa.
UKWELI
Kuongoka (Kugeukia maisha ya Mungu) ni kuchukuliwa mimba na sio kuzaliwa. Naamini imeeleweka vizuri sana. Mtu ambaye ameongoka, baada ya kutubu, akampokea roho mtakatifu,
uanza kubadilika kimawazo na nia (soma waef. 4:22-24) na hata tabia. Lakini mtu huyu huwa bado ni mwili wa nyama. Kuna kifungu ambacho kimeshangaza wengi na kuwafanya wafikirie kuwa Biblia inafarakana. Kinasema; “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi, kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu – 1 Yohana 3:9.” Je, si hiki kifungu kinapinga kingine katika 1Yohana 1:8 kinachosema; “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe; wala kweli haimo ndani yetu? Ili tuweze kuelewa; maana yake, lazima tufahamu kuwa, vifungu hivi vinaongea juu ya wakristo. Mtu akiisha zaliwa mara ya pili, akiwa roho, atakuwa ameshinda dhambi kabisa, hataweza kutenda dhambi. Lakini mtu akiongoka,
ijapokuwa roho wa Mungu yuko ndani yake, anaweza kutenda dhambi (soma 1 Yohana 1:9).
MKRISTO HATAKIWI KUTENDA DHAMBI
Kweli, Biblia inasomesha kuwa, mkristo hapaswi kutenda dhambi (soma 1 Yohana 2:1). Mkazo katika agano jipya yote ni kuwacha dhambi, kuishinda na kukuwa katika uhaki. vifungu vingi, na hasa katika Warumi 7:1 – 25 uonyesha kwamba katika haya maisha, mkristo mara kwa mara utenda dhambi, ijapokuwa sio kwa kupenda, mbali kwa kuteleza kinyurne cha mapenzi yake. Ijapokuwa Yesu hakutenda dhambi, alijaribiwa na kila aina ya
dhambi. Maandiko haisemi kuwa Yesu hangetenda dhambi, mbali, hakutenda dhambi.
Kulikuwa na uwezekano wa kutenda dhambi lakini akaishinda kabisa. Tukiisha jua hayo, ni wasi kwamba 1 Yohana 3:9 inaongea juu ya wakati tutakuwa tumezaliwa mara ya pili, sio
wakati huu wa sasa. (Soma 1 Yohana 3:1.2). Hii inazungumzia kuhusu wakati tutakuwa roho – wakati tutazaliwa mara ya pili.
TUTAKUWA WATU WA NAMNA GANI?
Sasa, angalia na uelewe vile tutakuwa wakati tutazaliwa mara ya pili. Pia uelewe wakati huo utakuwa lini. Katika 1Yohana 3:2, hiki kifungu kinasema vizuri sana kwamba, “sisi” tulio na roho
wa Mungu sasa, tulio ndani ya tumbo ya mama yetu wa Kiroho, tu wana wa Mungu. Lakini kuonyesha kweli bado hatujazaliwa, kifungu hicho kinaendelea kusema; “Wala haijadhihirika
(haijaonekana wasi) Bado tutakavyokuwa,” Umesikia hapo? Tukiisha zaliwa tena, tutakuwa tofauti na vile tulivyo sasa. Ndiyo, ijapokuwa tumechukuliwa mimba sasa, yaani tumepokea
roho mtakatifu, na tumekuwa wana wa Mungu, bado sisi ni mwili wa nyama. Hii ndio Yesu alimwelezea Nikodemu alipomwambia; “kilichozaliwa na mwili ni mwili, na kilichozaliwa na roho, ni roho. Kwa hivyo, wakristo bado hawajakuwa roho, bado hawajajua kabisa vile watakuwa wakiisha kuwa roho. Hata hivyo, 1 Yohana 3:2 anamalizia kwa kusema; “lakini twajua ya
kuwa, atakapodhihirishwa, tutafanana naye; maana tutamwona alivyo,” Ikiwa tunaweza kujua vile Kristo alivyo sasa kule mbinguni aliko, basi twaweza kujua vile tutakuwa tukiisha zaliwa
mara ya pili. Basi je; Kristo yukoje? Macho yake ni kama miali ya moto, miguu yake ni kama shaba iliyosuguliwa sana, sauti yake kama maji mengi, uso wake kama jua liwakalo adhuhuri (somo. Ufunuo. 1:14-16, 19:12-13; Mat. 17:2). kwa vile tutafanana naye, bila shaka, tutametameta vivyo hivyo baada ya kuwa viumbe wa roho kama yeye. Danieli anadhibitisha hayo akisema, “Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele – Dan. 12:3.”
Wandungu wapenzi, hivyo ndivyo tutakavyokuwa tukiisha zaliwa tena. Kweli hao ambao wamedanganyika na kusema tayari wamezaliwa; wana metameta sasa? Wakati umefika wa kondoo wa Mungu kutoka babeli na kuingia katika zizi lake. Hii ni dhihirisho wasi kwamba wakati wa kuzaliwa mara ya pili na kuvikwa mwili wa kiroho ni wakati wa mwisho , wakati. Yesu atarudi kuitawala hii dunia ambapo, atawafufua wakristo wote na kuwabadili wale walio hai; kuwapa mwili kama ule wake (soma Wafilipi 3:21).
JE UTAAMIN1 HUU UKWELl
Kweli, utaamini? Utakubali lile neno la Mungu linasema katika waebrania? Kwa nini Mungu anamshughulikia mwanadamu? Ukiangalia chini kutoka kwa ndege juu, utaona wanadamu
wakiwa wadogo kama mchwa. Ukienda juu zaidi kama maili nne, hutaweza kuona mtu. Je, unafikiria mtu ni kitu gani kwa Mungu ata ahusike naye? Jibu liko katika Waebrania 2:6, Mungu aliumba mtu kwa kiwango cha chini kuliko malaika. Lakini kwa mpango na kusudi lake, atamfanya mwanadamu kuwa mwenye utukufu mkuu kuliko malaika, kama alivyomfanya Yesu Kristo. Je, Kristo alitawazwa kwa utukufu gani? Kutawazwa kunahusu – utawala, mamlaka na kiti cha enzi. Kabla hajapaa mbinguni, Yesu aliwambia mitume; “Nimepewa mamlaka yote
mbinguni na duniani – Mat 28:18”. Katika Waebrania 1:1-3, Kristo anaonekana akiwa na mng’ao wa utukufu wa Mungu. Huo utukufu na mamlaka ya Yesu ni kiasi kwamba – nguvu zote, mamlaka na kila aina ya ukuu mbinguni na duniani zinamtii yeye. Nataka sasa uelewe vile Mungu anasema juu yetu wanadamu. “Kwa kuwa ilimpasa yeye ………. akilete wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya matezo.” Na tena; “haoni haya (Yesu) kutuita wandugu -Waebr. 2:10-11.” Tukiisha zaliwa mara ya pili, tutakuwa na utukufu na mamlaka kama hayo ya Yesu, lakini chini yake. (Soma Luka 12:44).
KWA NINI HATUNA HUU UTUKUFU SASA?
Kama inavyoonyesha katika Waebr. 2:8, hatuoni bado mtu yeyote ambaye amemiliki haya mamlaka na utukufu isipokuwa Kristo peke yake. Kwa nini basi hatujazaliwa bado? Maana,
tukiisha zaliwa tena, tutapewa nguvu na uwezo mwingi kiasi ambacho tunahitaji kufundishwa kuutumia kwanza na tuitimu kabla hatujakabidhiwa. Mungu ndiye muumba na mfalme juu ya
vyote. Hawezi kumkabidhi yeyote huo uwezo kabla huyo mtu hajajifunza na kushika njia zake (za Mungu) – yaani, kumtii. Kwa hivyo, ni wale tu watakaomtii, na kufuata njia zake, kutawala kulingana na maagizo ya ufalme wake na, chini ya uongozi wake, ambao Mungu atawapa hayo mamlaka. Kwa hivyo, ni wale tu wanaoongozwa na roho wa Mungu katika njia zake watakaofanyika wana wake War. 8.9. Na hao ni lazima wakue kwa kuyashinda mazoeya ya kimwili (soma 2 Wakor. 10:3- 4) na kumshinda shetani. Ni lazima kwanza tukue katika neema, na katika kumjua Bwana 2 Petro3:18” Kama vile mtoto aliye tumboni ukua kwa kula chakula kupitia kwa mama yake, ndio
akomae kiasi cha kuzaliwa, ndivyo inatupasa sisi Wakristo kulishwa kwa neno la Mungu kupitia kwa Kanisa, na kwa maombi, na kwa Kushirikiana na wandungu walio wa imani ya
kweli, baada ya kumpokea roho mtakatifu. Tusipoendelea kukua katika kufanana na Mungu, kwa njia ya kusoma na kutenda amri zake (na ni kwa uwezo wa huyo roho wake aliye ndani yetu), tutakuwa kama yule mtoto ambaye mimba yake utolewa, ama ikatoka kabla kuzaliwa, na hivyo hatutazaliwa mara ya pili. Tutakuwa tumeshindwa na tutapotea.
ULIMWENGU UJAO WA UTUKUFU
Habari njema ni kwamba, Yesu yukaribu kurudi hapa duniani. Muda mfupi tu, na huu ulimwengu wa utukufu utakuwa hapa. Wote ambao sasa wamepokea na kuongozwa na roho
mtakatifu watazaliwa, watoe huu mwili ufao na kivikwa mwili usiokufa, ndio – kutoka kwa uaribifu na kuvaa kutokuharibika. Huku kuzaliwa mara ya pili kutakuwa na utukufu ambao, wale
waliodanganyika ati sasa wamezaliwa kiroho hawawezi ata kuuelewa. Naamini umeona kile kinakungoja, kama utatubu na kuamini huu ukweli na kuutenda, Neno la Bwana ambayo
imetueleza hayo yote inatuonya ikisema; “…………. leo, kama mtaisikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu………….” “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambayo roho
anayaambia makanisa” Waebr.3:7-8; Ufu. 2:29.